jiunge na WeFarm

Karibu kwenye WeFarm: mtandao wa watu wasiokuwa na intanenti. WeFarm huwawezesha wakulima katika jamii za maeneo ya mashambani ulimwenguni kumpa kila mmoja elimu na usaidizi wa kilimo kupitia kwa intanenti na ujumbe wa SMS. Kupitia kwa huduma ya kipekee baina ya wakulima wenza, wakulima wanaweza kupata mbinu mpya za ubunifu katika lugha zao wenyewe ili kuboresha maisha yao na kuimarisha jamii zao.Kwa mfano: Mkulima nchini Uganda akigundua wadudu wanaoharibu mimea kwa sababu ya mabadiliko ya hivi karibuni ya hali ya anga na hakuna yeyote katika kijiji chake amewahi kuwaona wadudu hawa. Kupitia WeFarm anaweza kutafuta ushauri kwa ujumbe wa SMS na kupokea ushauri kutoka kwa mkulima wa ushirika aliye nchini Meksiko ambaye amekabiliana na wadudu hawa kwa miaka kadhaa. muhimu. Hata hivyo, mawasiliano haya hayawezekani bila watafsiri kama wewe ili kufanya maelezo haya yapatikane katika lugha yake mwenyewe. Kwa kujitolea kutafsiri maswali au majibu 5 tu kwa siku kokote ulipo ulimwenguni, utakuwa mmoja wa jumuiya ya wanafunzi, wataalam na wanaisimu wanaojihusisha katika miradi muhimu ya kubadilisha maisha.

Farmers