Jiunge na WeFarm

WeFarm ni huduma isiyolipishwa ambapo wanachama wanaweza kuuliza maswali na kushiriki mbinu na ushauri wa kilimo kwa kutumia jukwaa hili la mtandaoni au kwa kutuma ujumbe rahisi wa SMS unaotozwa gharama za nchi yao. WeFarm hutumia intaneti, na mfumo wetu wa kipekee wa kutafsiri wa wakulima wengine, kushiriki maarifa na wanachama wengine wa WeFarm kupitia SMS kote ulimwenguni. Ili upate maelezo zaidi kuhusu WeFarm na jinsi unaweza kuhusika, tembelea wefarm.org

Wakulima
Watafsiri

Kwa nini wakulima?

Kama mkulima unaweza kuuliza wakulima wengine kote ulimwenguni maswali, upokee ujumbe, au ushiriki maarifa kama mbinu kwa kutumia simu yako ya kawaida tu.

Kwa nini wafanyikazi wa Ushirika?

Kama mfanyikazi wa Ushirika, unaelewa matatizo yanayokumba jamii yako na unaweza kutumia WeFarm kama nyezo muhimu kusaidia wakulima katika ushirika wao.

Kwa nini Watafsiri?

Wakulima wetu huzungumza lugha nyingi tofauti, na mara nyingi hutumia misemo yao kama 'shamba' kumaanisha 'shamba' nchini Kenya, na mara nyingi huwa na maendelezo tofauti.